Sunday, August 25, 2013

muda mwingine urembo ukizidi unaweza haribu ngozi ya uso.

kutumia vipodozi kuweka usowako vizuri inapendeza lakini baadhi ya vipodozi ni vibaya kwa ngozi zetu.


urembo wa nyusi na kope.



ni moja kati ya dawa zinazotumika kuzifanya kope ziwe zimesimama na zenye kuvutia kwani hutumika wakati wa kuchana kope.



matumizi wa dawa hiyo huzifanya zionekane kama hivi.





pindi zikisha bandikwa huwa na muonekano kama huu wenye kuvutia.

 

kitu chakwanza cha kuhatarisha macho juu ya kubandika kope ni kusababisha upofu au uonaji hafifu kwani wakati unaweka kope bandia lazima utumie gundi kuzifanya zishikane na ngozi,

gundi zinazo tumiwa huwa na kemikali tofauti kwani kila kampuni ya kope wanajua watumie kemikali gani wakati wa kutengeneza gundi ya kustahimili aina ya kope waliyo itengeneza.





kope bandia huwa na muonekano huu kabla ya kubandikwa kwenye sehemu husika,







Moja kati ya vitu vinavyoleta muonekano mzuri wa uso wa mtu ni nyusi.lakini watu wengi wamekuwa wakitindo nyusi bila kujua madhara yake,nyusi ni moja kati ya vikinga uchafu ambao hutaka kuingia kwenye macho.

lakini watu wamekuwa wakitinda na kuzipunguza urefu wake kwa dhumuni la kuwa na muonekano mzuri